Inger Andersen

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na Naibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Read her speeches

Wasifu

Inger Andersen aliteuliwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres mnamo Februari mwaka wa 2019.

Kati ya mwaka wa 2015 na Mwaka wa 2019, Bi. Andersen alikuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Muungano wa Kimataifa wa Kuhifadhi Mali Asili (IUCN).

Bi. Andersen anaingia afisini akipendelea sana kuhifadhi mazingira na kuwezesha maendeleo endelevu. Hali hii inadhihirika kutokana na kufanya kazi kwa zaidi ya miaka 30 katika ukuzaji wa uchumi kimataifa, utunzaji wa mazingira na uundaji wa sera. Pia amefaulu kuanzisha na kuendeleza miradi inayozalisha matunda. Amekuwa mstari mbele kusaidia mataifa yanayozungukwa na maji kutunza mito na kutumia maji vizuri katika ngazi ya kimataifa.

Kabla ya kujiunga na (IUCN), Bi. Andersen alishikilia nyadhifa mbalimbali za uongozi katika Benki ya Dunia na katika Shirika la Umoja wa Mataifa. Hivi majuzi, alihudumu kama Naibu wa Rais wa Mashariki ya Kati na Kusini mwa Afrika katika Benki ya Dunia. Awali, alihudumu kama Naibu wa Rais wa Maendeleo Endelevu, na kama Mkuu wa Mfuko wa Kamisheni ya Vituo Vya Kimataifa vya Utafiti wa Kilimo (CGIAR). Kwa kipindi cha miaka 15 alipohudumu katika Benki ya Dunia, alisimamia miradi ya maji, mazingira na maendeleo

endelevu hasa katika maeneo ya Afrika na Mashariki ya Kati. Kabla ya kujiunga na Benki ya Dunia, Bi. Andersen alifanya kazi na Umoja wa Mataifa kwa miaka 12. Alianzia katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Sudano-Sahelian, akiwajibikia masuala yanayohusiana na ukame na majangwa kabla ya kuteuliwa kama Mratibu wa Maji na Mazingira wa Mpango wa Mandeleo wa Umoja wa Mataifa katika Eneo la Uarabu.

Historia ya Elimu ya Bi. Andersen ya kimasomo ni pamoja na Shahada ya kwanza ya BA kutoka Chuo Kikuu cha London Metropolitan University North na Shahada ya Uzamili ya MA kutoka School of Oriental and African Studies kutoka Chuo kikuu cha London, hasa akisomea ukuzaji wa uchumi.

Ингер Андерсен

Ungana na Inger Andersen


The Latest

Hotuba
Ni wakati wa kushughulikia mabadiliko ya tabianchi kikamilifu. Tukizingatia kiwango cha ongezeko la joto duniani, hakuna aliye salama.

Hotuba iliyoandaliwa kuwasilishwa katika mkutano wa waandishi wa habari kuzindua Muhtasari kwa Watungasera wa Kikundi Kazi I kuchangia Ripoti ya 6 ya Tathmini ya Jopo la Serikali Mbalimbali kuhusiana na Mabadiliko ya Tabianchi inayojulikana kama “Mabadiliko ya Tabianchi 2021: Msingi wa Sayansi Halisi.”   More

Hotuba
Kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira ni muhimu barani Afrika

Hotuba iliyoandaliwa kutolewa wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Utekelezaji wa Hatua za Kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira na Tume ya Umoja wa Afrika More

Video
Inger Andersen atoa wito wa amani kwa mazingira

Migogoro ya kujiami hudhuru mazingira. Juhudi za kimataifa ni muhimu mno ili kupata suluhu itakayonufaisha watu na sayari na kudumisha amani.   More