Tangu kuanzishwa kwake katika mwaka wa 1972, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ni mamlaka ya kimataifa inayoweka ajenda ya mazingira, linawezesha utekelezaji wa vipengele vya mazingira vya maendeleo endelevu kwenye mfumo wa Umoja wa Mataifa, na hufanya kazi kama mtetezi mkuu wa mazingira duniani.
Dhima ya UNEP ni kutoa uongozi na kuwezesha ushirikiano wa kutunza mazingira kwa kuhimiza, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuathiri yale ya vizazi vijavyo.
UNEP inafanya kazi ilikuleta mabadiliko chanya kwa watu na mazingira kwa kuangazia chanzo cha changamoto tatu duniani za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira na uharibifu wa bayoanuai, na uchafuzi na taka. UNEP inatumia programu ndogo saba zilizoingiliana kuchukua hatua: Kushughulikia Mazingira, Kushughulikia Kemikali na Uchafuzi, Kushughulikia Asili, Sera ya Sayansi, Kusimamia Mazingira, Mabadiliko ya Kifedha na Kiuchumi na Mabadiliko ya Kidijitali.
Kupitia kampeni zake, hususan Siku ya Mazingira Duniani, UNEP huhamasisha na kupigania ushughulikiaji mwafaka wa mazingira.
Na Makao Makuu yake mjini Nairobi nchini Kenya, UNEP hufanya kazi kupitia kwenye idara zake na pia kupitia katika ofisi zake za kikanda na kupitia kwa mtandao unaokua wa vituo vinavyoshirikia bora zaidi.
UNEP inafanya kwa ushirikiano na Nchi Wanachama 193 na wawakilishi kutoka mashirika ya kiraia, mashika ya biashara, na makundi mengine makuu na washikadau kushughulikia changamoto za mazingira kupitia Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa, taasisi ya ngazi ya juu zaidi inayofanya maamuzi duniani kuhusu mazingira.
Shirika hili ni mwenyeji wa sekretarieti za mikataba mingi muhimu kuhusu mazingira na mashirika ya utafiti.
Mkurugenzi Mtendaji na Kikosi cha Wasimamizi Wakuu wanaongoza utekelezaji wa Mkakati wa Muda (MTS) wa UNEP. MTS ya miaka minne inaelezea wajibu wa UNEP katika kutekeleza ahadi za Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu na Kongamano la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Endelevu (Rio+20) pamoja na hati ya matokeo yake, “Hatima Tunayoitaka.”
UNEP husaidia Nchi Wanachama kuhakikisha kwamba zinajumuisha uendelevu wa mazingira katika mipango ya maendeleo na uwekezaji na hutoa kwa nchi zana na teknolojia muhimu za kutunza na kuboresha mazingira. Kazi yake hufanikishwa na wabia wanaofadhili na kutetea dhima yetu. UNEP inategemea michango kutoka kwa wahisani kwa asili mia 95 ya mapato yake.